Wasiwasi kuibuka mapambano mapya kati ya Israel na Parestina.
Mzozo kati ya Israel na Palestina unazidi kushtadi baada ya waisrael wawili kuuliwa na vijana wa kipalestina kwa kuchomwa visu huku Palestina ikijiandaa kuadhimisha miaka kumi tangu kufariki kwa kiongozi wa nchi hiyo madhulumu Yasser Arafat
Maombolezi ya miaka kumi tangu kifo cha kiongozi wa Palestina aliyeenziwa Yasser Arafat yamefutiliwa mbali katika ukanda wa Gaza kutokana na sababu za kiusalama lakini yanatarajiwa kufanyika katika ukingo wa magharibi.
Kiongozi huyo anayekumbukuwa kwa kutia saini makubaliano ya amani ya Oslo mwaka 1993 na Israel, alifariki dunia mwaka 2004 katika hospitali moja mjini Paris akiwa na umri wa miaka 75.
Chanzo cha kifo chake kimeleta sintofahamu kati ya waparestina na waisrael, ambapo uchunguzi uliofanywa na waparestina unathibitisha kuwa kiongozi huyo aliuawa kwa kuwekewa sumu aina ya Polonium na utawala wa Israel
Maadhimisho hayo yanakuja huku hali ya kiusalama kati ya wapalestina na waisrael ikizidi kuwa tete. Waisrael wawili hapo jana waliuliwa kwa kuchomwa kisu na vijana wanaosadikiwa kuwa ni wapalestina katika matukio mawili tofauti.
Katika tukio la kwanza, kijana wa kipalestina alimdunga kisu tumboni, mwanajeshi mmoja wa Israel mwenye umri wa miaka ishirini katika ukingo wa magharibi ambaye alifariki baadaye akiwa hospitalini.Mshambuliaji aliyetambulika kwa jina Nureddine Abu Hashiyeh mwenye umri wa miaka 17 alitoroka lakini baadaye alikamatwa.
Saa chache baadaye,mpalestina mwingine aliwashambulia waisrael watatu waliokuwa katika kituo cha magari kusini mwa ukingo wa magharibi na kumuua mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 25 na kuwajeruhi vibaya wengine wawili kabla ya kupigwa risasi na mlinzi aliyemjeruhi vibaya.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netayanyahu ameapa kukabiliana vilivyo na vitisho vinavyolenga kuhataraisha maisha ya waisrael
Mashambulizi hayo yamelaaniwa vikali na Marekani na Umoja wa Ulaya.Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Jen Psaki amesema ni muhimu kwa pande zote kuchukua hatua zinazofaa kuwalinda raia na kupunguza mzozo kati yao.
Ofisi ya mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini imeonya hali huenda ikazidi kuzorota kati ya Israel na Palestina kutokana na kutokuwepo kwa nia ya kisiasa kuumaliza mzozo.
Israel imesema inaimarisha usalama katika miji yote mikubwa na katika ukingo wa magharibi kufuatia mashambuliuzi hayo .Msemaji wa polisi Micky Rosenfeld amesema vikosi vya usalama vimetumwa katika miji kadhaa ikiwemo Tel Aviv na Jerusalem kukabiliana na mashambulizi zaidi.
Tangu mwezi Julai askari wa Israel wamewakamata wapalestina 900 kwa kuvuruga amani mashariki mwa Jerusalem na thuluthi moja kati yao wamefunguliwa mashitaka.
Inafaa kuashiria kwamba kumekuwa na matukio ya visasi kati ya Israel na Parestina ambapo Israel inaongoza kwa kuwaua waparestina.